Welcome To Our Official Website

ASKARI POLISI WANNE WAFUKUZWA KAZI SHINYANGA

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini Ernest Mangu

Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga limewafukuza kazi askari polisi wake wanne wakiwemo watatu wa kikosi cha usalama barabarani ambao wamefukuzwa kwa kosa la kupokea rushwa na kwenye magari barabarani na askari mwingine kwa kosa la utoro jeshini baada ya kujipa likizo mwenyewe.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga kwa vyombo vya habari iliyotolewa Juni 16 ,2014  na kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga kamishina msaidizi wa polisi Kihenya Kihenya.

Kamanda Kihenya amesema kwa mujibu wa mamlaka aliyokasimiwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IJP amewafukuza kazi askari polisi hao kwa fedheha kuanzia Juni 11,2014 kwa kosa la kufanya kitendo kibaya kinyume na mwenendo mwema wa jeshi la polisi cha kupokea rushwa wakiwa kazini tarehe 30,Machi,2014 majira ya mchana.

Kamanda Kihenya amewataja askari wa kikosi cha usalama barabarani waliofukuzwa kazi kuwa ni EX.F.899 koplo Jonathan James Bujiku,EX.WP.5198 Pc Joyce Malima Paul na EX.F 9839 pc Sohela Mabeho Kisinza.

Amesema askari hao walipokea rushwa ambayo thamani yake haikufahamika kutoka kwa kondakta,wahusika wa magari tofauti wakiwa kazini katika barabara kuu ya Shinyanga –Tinde eneo la Nhelegani katika manispaa ya Shinyanga.

Jeshi hilo la polisi pia limemfukuza kazi kuanzia Juni 12,2014 askari polisi EX.G.3829 pc Prosper Kayaya wa kazi za kawaida kwa kosa la utoro jeshini ambapo askari huyo alijipa likizo.


Kamanda Kihenya amekemea vitendo hivyo kwani ni kinyume cha mwenendo mwema wa jeshi la polisi huku akiwataka askari wa jeshi la polisi mkoani Shinyanga kufanya kazi kwa uwazi,uaminifu na uadilifu mkubwa.

CHAMA CHA BAISKELI TANZANIA CHAWASIMAMISHA VIONGOZI WAKE WAWILI KWA UTOVU WA NIDHAMU

Mwenyekiti wa chama cha Baiskeli nchini(CHABATA) Godfrey Jax Mhagama akizungumza na waandishi wa habari  mjini Shinyanga kuzungumzia maamuzi yaliyofikiwa na kikao cha kamati ya utendaji taifa ya CHABATA iliyoketi Juni 15,2014 mkoani Shinyanga
Kaimu mwenyekiti wa CHABATA taifa Simon Tungu Jackson akisisitiza jambo katika kikao hicho  mjini Shinyanga
Wa kwanza kulia ni katibu mkuu wa CHABATA John Machemba akizungumza katika kikao chao na waandishi wa habari mjini Shinyanga 

Waandishi wa habari wakifuatilia kilichokuwa kinazungumzwa na viongozi wa Chama cha Baiskeli nchini (CHABATA) 

Waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio
Kamati ya tendaji ya chama cha Baiskeli taifa (CHABATA)  imewasimamisha wajumbe wake wawili kutokana na utovu wa nidhamu  waliouonesha ndani ya chama kama vile kusambaza taarifa za uongo katika vyombo vya habari ikiwemo kudai kuwa viongozi wa ngazi ya juu wa CHABATA wametafuna shilingi milioni 26 za mdhamini ambaye hata hivyo wajumbe waliosimamisha wamekuwa hawataji ni wadhamini gani.

Akizungumza wakati wa kikao cha kamati hiyo tendaji ya Chabata taifa na waandishi wa habari mjini Shinyanga mwenyekiti wa chama cha Baiskeli nchini Godfrey Jax Mhagama amesema maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha kamati tendaji ya CHABATA iliyokaaa Juni 15,mwaka huu mjini Shinyanga.

Mhagama amesema miongoni mwa mambo yaliyoazimiwa katika kikao hicho ni kwasimamisha viongozi wawili ambao ni Lucas Bupilipili aliyekuwa katibu mkuu wa CHABATA mkoa wa Mwanza na Moses Andrew aliyekuwa kiongozi katika moja ya klabu ya baiskeli mkoani Arusha.

Amesema viongozi hao kuanzia sasa hawataruhusiwa kujishirikisha michezo ya baiskeli na kuzungumzia chochote kuhusu michezo ya mpaka pale utakapofanyika mkutano mkuu wa CHABATA ambao utatoa maamuzi kuhusu kusimamishwa kwa wajumbe hao.

Katika hatua nyingine Mhagama amesema kikao hicho cha mwisho katika nusu ya mwaka kilifanya mabadiliko ya katiba ya chama ambapo wameongeza kamati ya uongozi na sasa chama cha Baiskeli Zanzibar (CHABAZA) kimeingizwa katika chama cha Baiskeli Tanzania(CHABATA) na tayari walishafanya mazungumzo na CHABAZA kuhusu maamuzi hayo.

Mhagama amesema kikao hicho cha kamati tendaji kimemteua rasmi Kamanda Suleiman Kova kuwa mlezi wa chama huku wakili Magusu Mugoka akiteuliwa kuwa mwanasheria na Charles Kuziganika kuwa mhasibu wa CHABATA.

Aidha kikao hicho pia kimeteua wajumbe wawili wa baraza la wadhamini ambao ni mzee Shaaban Masamaki Bwire na mzee Leonard Derefa aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini mkoa wa Shinyanga.

Naye katibu mkuu wa CHABATA John Machemba ametumia fursa hiyo kuwaasa wajumbe wa chama hicho kufuata taratibu zinazotakiwa katika chama na kwamba hivi sasa chama kimejipanga vizuri kama taasisi kufanikisha malengo yao katika kuhakikisha kuwa CHABATA inafanikiwa hadi ngazi ya kimataifa.


Machemba amesema pamoja na kuwepo kwa tuhuma nyingi dhidi ya chama hicho mambo mengi zaidi watayawasilisha katika mkutano mkuu wa chama ambao watautumia kuwaeleza wapenzi wa baiskeli na watanzania kwa ujumla kuhusu mambo yanayoendelea katika chama na mchezo wa baskeli kwa ujumla

Na Kadama Malunde-Shinyanga

OUR ADVITICEMENT COSTS AT RADIO FARAJA FM STEREO 91.3



CATHOLIC DIOCESE OF SHINYANGA
RADIO FARAJA FM STEREO 91.3 Mhz


  
Tel:   +255 28 276 2633                                                           P.O. BOX 47
Mob: +255 759 904 774                                                           SHINYANGA
Email:         skidaha4@yahoo.com                                                  TANZANIA.
Website: www.radiofaraja.com



AIR TIME CHARGES
(20% VAT EXCLUSIVE)



A.            PRIME TIME
Commercial Rate
Duration of a Programme
Cost
60 seconds
42,000/=
45 seconds
38,000/=
30 seconds
36,000/=
15 seconds
30,000/=

Casual Advert
Duration of a Programme
Cost
60 seconds
30,000/=
45 seconds
26,000/=
30 seconds
22,000/=
15 seconds
18,000/=

B.            ORDINARY TIME
 Commercial Rate
Duration of a Programme
Cost
60 seconds
26,000/=
45 seconds
22,000/=
30 seconds
18,000/=
15 seconds
14,000/=

Casual Rates
Duration of a Programme
Cost
60 seconds
20,000/=
45 seconds
16,000/=
30 seconds
12,000/=
15 seconds
  8,000/=

C.       COMMERCIAL RATE FIVE MINUTES BEFORE
       AND AFTER RF AND DW NEWS PROGRAMMES
Duration of a Programme
Cost
60 seconds
100,000/=
45 seconds
85,000/=
30 seconds
60,000/=
15 seconds
45,000/=






D.       PROGRAMME SPONSORSHIP
Duration of a Programme
Cost
60 seconds
150,000/=
45 seconds
125,000/=
30 seconds
100,000/=
15 seconds
75,000/=

E.       AIR TIME CHARGES e.g. OB, MASS,
       CAMPAIGN, SEMINAR, etc
Duration of a Programme
Cost
60 minutes
300,000/=
45 minutes
200,000/=
30 minutes
150,000/=
15 minutes
100,000/=

F.       PROMOTIONS e.g. A PRODUCT, SERVICES
Duration of a Programme
Cost
07:00 – 09:00  
500,000/=
09:00 – 13:00
700,000/=
14:00 – 16:00
350,000/=
16:00 – 18:00
400,000/=
19:00 – 21:00
500,000/=
21:00 – 23:00
450,000/=


SPONSORING PACKAGE
Five sponsors promo will be aired during the program with 2 bonus spots per day,
Sponsor will be allowed to introduce any of new promo and granted with interviews,
Radio Faraja will cover the sponsor’s events in its daily news bulleting.

                                                    BONUS
Radio Faraja Fm guarantees to give a bonus of two adverts a day.

With much regards,



Padri Slivanus Kidaha
Director Radio Faraja

KARIBU REDIO FARAJA FM

Radio Faraja FM inayofuraha kuwakaribisheni nyote katika website yake itakayokupatia taarifa zote zinazoihusu redio yetu na matukio mbalimbali yanayofanyika katika vipindi vya redio yetu.